Na Mapuli Kitina Misalaba
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Stephen Julius Masele, leo Juni 28, 2025, amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Masele, ambaye amewahi kuhudumu kwa muda mrefu katika nafasi za kitaifa na kimataifa, amechukua fomu hiyo katika ofisi ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini na kueleza dhamira yake ya kuendelea kulitumikia jimbo la Shinyanga Mjini kwa msukumo mpya wa maendeleo.
Stephen Masele alihudumu kama Mbunge wa Shinyanga Mjini kuanzia mwaka 2010 hadi 2020, ambapo alijipatia umaarufu kutokana na ushawishi wake ndani na nje ya nchi kupitia nafasi yake ya kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, akiwakilisha Tanzania katika jukwaa hilo la bara.
Kwa sasa, macho na masikio ya wakazi wa Shinyanga Mjini yanakodolewa kuelekea mchakato wa uteuzi wa mwisho ndani ya CCM ili kubaini iwapo mwanasiasa huyo mkongwe atapata nafasi ya kurejea tena bungeni.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment