" AJALI YA MOTO SHINYANGA: BIBLIA NA MAFUTA YA UPAKO YABAKI SALAMA

AJALI YA MOTO SHINYANGA: BIBLIA NA MAFUTA YA UPAKO YABAKI SALAMA

NYUMBA YA MWALIMU YATEKETEA KWA MOTO KIZUMBI, SHINYANGA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Nyumba ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Ishinabulanda, Manispaa ya Shinyanga, imeteketea kwa moto Agosti 27, 2025 majira ya saa sita mchana na kusababisha uharibifu wa mali mbalimbali.

Moto huo uliteketeza vifaa na mali za thamani zikiwemo kitanda, vyakula na nguo, huku thamani kamili ya hasara ikiendelea kufanyiwa tathmini.

Mmiliki wa nyumba hiyo, Mwalimu Mathias Balele, amesema ingawa hajabaini ukubwa wa hasara, chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme.

Walimu wa shule hiyo waliokuwa shuleni wakati wa tukio wamesema waliona moshi ukipanda juu ya nyumba hiyo na kusikia sauti za kuomba msaada kutoka kwa mfanyakazi wa ndani, ndipo wakaungana na wananchi kujaribu kuzima moto kabla ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufika.

Jeshi hilo lilifika kwa wakati na kufanikiwa kuuzima moto huo kabla haujasambaa katika nyumba za jirani.

Cha kushangaza, katika tukio hilo, Biblia pamoja na mafuta ya upako vilibaki salama bila kuungua, licha ya moto huo kuteketeza mali nyingine zote.Biblia pamoja na Mafuta ya upako yavikuungua katika ajali hiyo ya moto.Mwalimu Mathias Balele, akizungumza na Misalaba Media.


GUSA LINK HAPA CHINI👇


APPLICATION FORM

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 



 

Post a Comment

Previous Post Next Post