" WANANCHI IPARAMASA WAMSHUKURU PASCHAL LUTANDULA KWA KUFANIKISHA MFUMO WA MAJI TAKA KWENYE KITUO CHA AFYA

WANANCHI IPARAMASA WAMSHUKURU PASCHAL LUTANDULA KWA KUFANIKISHA MFUMO WA MAJI TAKA KWENYE KITUO CHA AFYA




 



Wananchi wa Kata ya Iparamasa, Wilayani Chato mkoani Geita wamemshukuru Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, Paschal Lutandula, kwa kufanikisha ukamilishaji wa mfumo wa maji taka katika wodi ya wazazi kwenye Kituo cha Afya cha Iparamasa, uliokuwa umekwama kwa zaidi ya miezi sita.

 

Kukwama kwa mfumo huo kulisababisha wanawake kutumia choo kimoja kwa pamoja na wanaume, hali iliyozua usumbufu na kero kubwa hasa kwa akinamama wajawazito na waliojifungua. Hata hivyo, baada ya jitihada za Lutandula, kazi hiyo ilikamilika ndani ya wiki moja na vyoo hivyo kukabidhiwa rasmi kwa wananchi.

 

Wananchi kwa furaha kubwa walimlaki Lutandula kwa bashasha, nyimbo za shukrani na vifijo, wakieleza kuwa hatua hiyo imeondoa usumbufu mkubwa waliokuwa wakiupata kwa muda mrefu.

 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya kituo hicho, John Buswelu, alisema:

 

“Wananchi, hususan akinamama wajawazito na waliojifungua, walikuwa wakipata shida kutumia vyoo vya nje. Tulifikisha kilio chetu kwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu na ndani ya wiki moja alihakikisha mfumo huo unakamilika.”

Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Rechol Holomi, alieleza kuwa upatikanaji wa mfumo wa maji taka ni hatua kubwa katika kuboresha mazingira ya huduma kwa akinamama, hususan kipindi cha ujauzito na kujifungua.

Baadhi ya wananchi pia walitoa shukrani zao kwa Lutandula na kuwataka wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano wake wa uzalendo na kujitolea katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa kawaida.

Post a Comment

Previous Post Next Post