Yanga Yakataliwa na Mahakama Sakata la Dabi, Wapeleke tu Timu Uwanjani…
“Katika hatua inayoonekana kama muendelezo wa kushindwa kwa klabu ya Yanga kwenye vita yake ya kupinga maamuzi yaliyofanywa na Bodi ya Ligi Kuu nchini ya kughairisha mechi yao dhidi ya Simba SC hapo tarehe 8 Machi 2025, baadae kuipangia tarehe 15 Juni 2025. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu ya Dar es Salaam amewapa ushindi TFF na Bodi ya Ligi na kuamura gharama za kesi kulipwa na mlalamikaji ambaye mwanachama wa Yanga SC”
.
“Mwanachama wa Yanga SC Dr. SAMWEL JOHN MARWA mwenyeji wa Iringa mwenye kadi namba TZIRI03003030 mkazi wa Iringa Mjini alifungua kesi namba 9484 ya mwaka 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masija la Kuu ya Dar, ambayo ilikuwa chini ya Jaji MKWIZU E.Y.”
“Katika madai yake Dr. Marwa aliiomba Mahakama Kuu kuipa Yanga SC alama 3 na mabao 3 na pia kuizuia Bodi ya Ligi Kuu kuipangia tarehe nyingine ya kuchezwa mechi namba 184 kati ya Yanga na Simba, mchezo ambao Bodi umepanga uchezwe Juni 15,2025.”
.
“Jaji Mkwizu akinukuu vifungu kadhaa vya kanuni za ligi Kuu, Katiba ya TFF (ambayo Yanga ni mwanachama), Katiba ya Yanga (ambayo Dr. Marwa ni mwanachama) amesema Mahakama yake HAINA MAMLAKA kuisikiliza kesi hiyo na mamlaka hayo yapo TFF, CAS na vyombo vingine vya soka ambavyo katiba ya Yanga imevitambua, kuvitii na kuwataka wanachama wake kuvitii kuvitambua na kutopeleka masuala ya mpira katika Mahakama za kiraia/Mahakama za kisheria za kawaida. (Angalia slides ambatanishi)”
NOTE: Yanga SC katika shauri hili washapigwa TKO (Technical KnockOut) na CAS.
“KILA KICHAKA KINAKATWA
Katika hali nyingine ni kama kila eneo Yanga SC linalokaribia kuwafanya “WASICHEZE NG’OO” na wasichukuliwe hatua linashindwa, wamebakiza nani atafanya maandalizi ikiwemo kuomba kiwanja, vitisho vya Mzee Msimu na genge lake akina Shabani Uda au wasiende halafu wachapwe na rungu la TFF wakiwa wameukosa na ubingwa.”
Post a Comment