Na Mwandishi wetu, MISALABA MEDIA
Agnes Mwandu, mkazi wa kijiji cha Kalagwa, amenusurika kifo baada ya kujifungua salama katika mti wa muembe, kwa msaada wa abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Kahama kuelekea Kakola.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa tano asubuhi, maeneo ya karibu na kijiji cha Ngaya, baada ya mama huyo kushikwa na uchungu akiwa njiani kuelekea kituo cha afya.
Mashuhuda wamesema kuwa Gari hiyo ilisamama ghafla baada ya mama huyo kuanza kuumwa sana, ndipo abiria wakashirikiana kumsaidia kujifungua mtoto wa kike akiwa chini ya muembe.
“Kama siyo wale abiria kuonyesha utu na upendo, huenda mama huyu na mtoto wake wasingesalimika,” amesema mmoja wa mashuhuda.
Post a Comment