Edwin Soko
Kahama, Shinyanga
Kampuni ya madini ya Barrick imekuwa mstari wa mbele kwenye kusogeza mbele mustakabali wa elimu Kwa kupitia ubia na Twiga.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mark Bristow alisema hayo kwenye mkutano wake na Vyombo vya habari kueleza mafanikio ya awamu wa pili ya Mwaka 2025 uliofanyika kwenye mgodi wa Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga wiki iliyopita.
Bristow alibainisha kuwa, Barrick kupitia ubia na Twiga Kwa pamoja wamewekeza dola milioni 30 Kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya Rais . Mpango huo unalenga kupanua miundombinu ya shule Nchini.
Aliongeza kuwa, mpango huo sasa upo kwenye awamu ya pili , unatarajiwa kuwapatia vyumba vya madarasa wanafunzi zaidi ya 45,000.
Naye Meneja wa Nchi Tanzania Melkiory Ngido alibainisha kuwa, Kampuni ya Barrick imeendelea pia kutekeleza miradi mbalimbali chini ya mpango wa kusaidia jamii(CSR) na jamii kunufaika kwenye maeneo mbalimbali kama ujenzi wa barabara ya Kahama hadi kakola Kwa kiwango Cha lami Kwa kilomita 73 .
Ngido ameweka bayana kuwa ubia na Kampuni ya Twiga umesaidia kwenye kupunguza matukio ya kiusalama na sasa hali ni shwari tofauti ilivyokuwa mwanzo.
Post a Comment