" DORINA OKANGA AJITOSA KUWANIA UBUNGE KUPITIA KUNDI LA VIJANA TAIFA

DORINA OKANGA AJITOSA KUWANIA UBUNGE KUPITIA KUNDI LA VIJANA TAIFA

Dorina Peter Okanga, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa kutoka Mkoa wa Shinyanga, (kushoto) akipokea fomu ya kuwania ubunge kupitia Kundi la Vijana Taifa kutoka kwa afisa wa UVCCM katika ofisi za umoja huo mkoani Shinyanga, Julai 1, 2025.

DORINA OKANGA AJITOSA KUWANIA UBUNGE KUPITIA KUNDI LA VIJANA TAIFA

Na Mapuli Kitina Misalaba

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa kutoka Mkoa wa Shinyanga, Muuguzi katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama na Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Kahama, Dorina Peter Okanga, leo Julai 1, 2025, amechukua fomu ya kuwania ubunge kupitia Kundi la Vijana Taifa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dorina ambaye pia ni kada wa chama hicho, amechukua fomu hiyo katika ofisi za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mkoa wa Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya kuomba ridhaa ya chama ili awawakilishe vijana bungeni na kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Zoezi hilo limefanyika kwa kufuata taratibu zote za chama, ambapo wagombea wote wanapaswa kuchukua na kurejesha fomu zao kabla ya hatua nyingine za mchujo kuendelea.MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa kutoka Mkoa wa Shinyanga, Muuguzi katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama na Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Kahama, Dorina Peter Okanga.

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post