
Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Kagera
Mchumi na mkulima Evance Kamenge kutoka mkoani Kagera ametoa pongezi kwa madiwani viti maalum walioguliwa julai 20, 2025 Mkoani Kagera na kuwa ushiriki wao ni hatua ya uthubutu wa hali ya juu sana.
Kamenge ametoa pongezi hizo na kusema kuwa washiriki hao na kuwa wameonyesha nia kubwa na kuwa sehemu ya maamuzi ya kubadilisha jamii.
"Mimi kama mtu ambaye nimekuwa nikijitokeza mara kadhaa katika kuwania nafasi ya ubunge kwa vipindi tofauti na ambaye kwa sasa ni mtia nia ubunge Jimbo la Missenyi mwaka 2025 nipende kuwashukuru akina Mama ambao bado wanaonyesha moyo wa kuyapigania maendeleo yetu"alisema Kamenge
Ameongeza kuwa kipindi hiki cha uchaguzi si cha kumnufaisha mtu mmoja bali ni kipindi cha kuinufaisha jamii huku akiwahimiza ambao hawakubahatika kupata nafasi hizo kutokata tamaa kwani mafanikio yapo mbele.
Mchumi huyo amesema wanaochaguliwa na hata ambao wamekosa nafasi kwa kipindi hiki wajue kwamba hao waliopewa nafasi wamepewa deni la kwenda kulipa maendeleo kwa wananchi na hao waliokosa kwa kipindi hiki wamuombe mwenyezi Mungu watafanikiwa kwa
kipindi kingine.
"Kwa moyo mkunjufu sana niwapongeze sana wale walishiriki, niwapongeze sana waliopiga kura niwapongeze sana walioshinda na sasa wasubiri baraza litakapokuwa limepatikana na hata mbunge na mwakilishi wao wa Jimbo kwa maana kikao kikubwa cha Nchi cha bunge tuamini sasa Missenyi inaweza ikawa mpya kama ambavyo imepata jina jipya la Jimbo.
Amesema kuwa ikitokea yeye akafanikiwa kupata nafasi ya kuwania kiti cha ubunge atahakikisha lengo lake linauwa ni kuleta fikra mpya hasa za kiuchumi ambazo zinaweza kusaidia jamii kutoka hapo ilipo kwenda hatua nyingine na kuwa hana shaka watashirikiana sana kujenga hoja madhubuti katika baraza la madiwani na atakuwa mstari wa mbele atakapopata nafasi.
Amesema kuwa atahakikisha pia analeta akili mpya kwenye Baraza la madiwani ikiwa ni pamoja na kwenda kupeleka mawazo yatakayokuwa yanatokana na wananchi kupitia madiwani wa viti maalum, madiwani wa kata na kuitisha mikutano ya mara kwa mara kwa wananchi kupeleka uwakilishi wao katika vyombo vya dola na kupeleka uwakilishi wao katika mataifa mbali mbali namna ya kufungua fursa kwa wananchi wake.
Aidha ameongeza kuwa endapo mwenyezi Mungu atabariki na kupampa nafasi ya kuwaongoza wana Missenyi atabuni mbinu mpya za namna ya kwenda kuwahudumia huku akitegenea matokeo makubwa zaidi kuliko sasa.
"wale waliojitokeza na hawakuweza kupata nafasi amezidi kuwapongeza na kuwa ni bora kushindwa kupata matokeo kuliko kushindwa kujaribu kuyatafuta matokeo"alisema Kamenge.
"Hawa ni washindi kwa sababu wameshinda hatua ya kwanza ya kujaribu na kwenda kuyatafuta matokeo na kuyapata ambapo matokeo yanakuja mara baada ya kujaribu mara nyingi hivyo niwatie moyo kwamba bado wanayo nafasi ya kutumika kwenye nafasi hizo walizonazo wajasiliamali, watumishi wanayo nafasi ya kuendelea kuitumikia jamii pia wanayo nafasi tena kipindi kingine kijacho" alisema mchumi huyo.
Hata hivyo amewasihi wananchi kuwa watulivu na kusubiri kuona vikao vya chama cha mapinduzi (CCM)vikileta wagombea huku akikiomba chama chake kuwachuja wagombea nafasi za ubunge kwa hoja zao na historia zao kwenye utendaji, na mipango waliyonayo.
Aidha amesema kuwaTaifa kwa sasa linahitaji kuingia kwenye mapambano halisi ya uchumi wa wananchi hasa mwananchi mmoja mmoja.
Pia amesema kuwa wananchi wanayo nafasi ya kuwa sehemu ya kuchagua viongozi watakaoweza kuwafikisha kwenye azma ambayo watu wote wanaiwaza na wanaikusudia.
Post a Comment