
Na: Belnardo Constantine, Misalaba Media
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amemfuta kazi waziri wa elimu ya juu wa nchi hiyo
Waziri huyo ametajwa kwa jina la Nobuhl Ambaye hivi karibuni alikabiliwa na matatizo ufisadi,uongo na hujuma baada ya chama muhimu katika serikali yake ya umoja wa kitaifa kufungua mashtaka ya jinai kikimtuhumu kwa kusema uongo mbele ya bunge.
Hatahivyo Rais Ramaphosa amekuwa akishinikizwa zaidi katika miezi ya hivi karibuni kumwondoa kazini waziri huyo, baada ya mawaziri kadhaa kutoka chama chake cha African National Congress (ANC) waliomtuhumu kwa ufisadi, hali ambayo imeongeza mvutano ndani ya muungano wa vyama kumi unaotawala taifa hilo.
Sambamba na Hilo Chama cha pili kwa ukubwa serikalini, Democratic Alliance (DA), mapema mwezi huu kiliwasilisha malalamiko kikimtuhumu Waziri Nobuhle Nkabane kwa kusema uongo mbele ya bunge ili kuficha uteuzi wa udanganyifu wa watu wanaohusishwa na ANC katika bodi za mamlaka ya elimu.
kutokana na tuhuma hizo Rais Cyril Ramaphosa amemwondoa Dkt. Nobuhle Nkabane katika wadhifa wa Waziri wa Elimu ya Juu na Mafunzo
Taarifa hiyo itolewa na ikulu ya Africa kusini katika taarifa ya usiku wa Jumatatu, baada ya Nkabane kushindwa kuhudhuria mikutano muhimu ya bunge ambapo alitarajiwa kutoa ufafanuzi kuhusu uteuzi wenye utata..
Post a Comment