Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Shirika la FOHOW Tanzania limeendesha semina ya tiba ya dawa asili za Kichina yenye lengo la kutoa elimu kuhusu tiba mbadala kwa magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya macho, kisukari, presha na kiharusi, huku wakisisitiza matumizi ya tiba hiyo kama njia salama na ya uhakika kwa Watanzania wanaosumbuliwa na maradhi sugu.
Akizungumza wakati wa semina hiyo, Said Hamis Said, kiongozi wa FOHOW Tanzania amesema bidhaa zao za tiba asili zimeendelea kuwasaidia watu wengi nchini, huku mashuhuda kutoka mkoa wa Shinyanga wakitoa ushuhuda wa kupona maradhi yaliyokuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu.
Kwa upande wake, Margreth Mbao, ambaye ni mmoja wa mawakala wa usambazaji wa bidhaa za FOHOW amesema tiba hiyo imethibitishwa na wataalamu na haina madhara kwa mtumiaji, akiwashauri wananchi kutumia fursa hiyo kuondokana na mateso ya maradhi yanayowakabili.
“Tumeshuhudia mabadiliko makubwa kwa watu waliotumia dawa hizi. Tunashauri watu waje wajifunze, waelewe na wachukue hatua ya kujikinga au kujitibu kwa njia salama ya asili,” amesema Margreth.
Aidha, FOHOW imetangaza kuwa tawi lake jipya la Shinyanga litafunguliwa hivi karibuni, hatua ambayo inatarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa mkoa huo na maeneo ya jirani.
FOHOW ni shirika linalojihusisha na usambazaji wa bidhaa za tiba asili kutoka China, na limejipambanua kwa kutoa suluhisho mbadala kwa afya ya jamii kupitia elimu na huduma za kiafya.
Kiongozi wa FOHOW Tanzania Said Hamis Said, akiendelea kutoa elimu katika semina hiyo.
Post a Comment