Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kupokea taarifa za kutekwa na kurejeshwa kwa mwanamke aliyejitambulika kwa jina la Christina Hezroni Polepole Kinyangazi, mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Bahari Beach, mtaa wa Katumba, Kinondoni.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro tukio hilo lilianza kuripotiwa kupitia mitandao ya kijamii mnamo Julai 17, 2025, ambapo mtu aliyejitambulisha kwa jina la Humphrey Polepole alidai kuwa dada yake alichukuliwa na watu wasiojulikana waliovamia nyumba yake kwa kuruka ukuta.
“Dada huyo alifika katika kituo cha Polisi Kawe na kutoa taarifa zinazohusiana na yeye kuchukuliwa na watu ambao hakuwafahamu na baadae walimrudisha nyumbani kwake jana hiyohiyo”, ameeleza Muliro.
Jeshi hilo limethibitisha kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na vyombo vingine vya usalama, huku likitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za uchunguzi zikiendelea.
Mapema leo Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo ametoa taarifa ya watu kuruka ukuta nyumbani kwa Dada yake na simu ya Dada yake haipatikani.
Hata hivyo, Polepole amesisitiza kuwa leo saa tano asubuhi atafanya “Press” yake kama kawaida.
Polepole ameitisha Mkutano na Waandishi wa Habari leo siku ya tarehe 18 Julai 2025, saa 5 asubuhi.
Polepole ametoa wito huo kupitia akaunti yake ya instagram, ambapo amesema kuwa ataifafanua barua aliyomuandikia Mhe. Rais kwa hatua na kwa maana njema ili kuondoa upotoshaji.
Polepole amekanusha kutafuta maisha nje ya Tanzania, na kusema “jambo hilo halipo katika fikra zangu za jana, leo na kesho.”Polepole akanusha madai ya kuomba hifadhi nje ya nchi: Kuondoka Tanzania ni jambo ambalo sitokaa nilifanye.
Post a Comment