" KATIBU TAWALA WILAYA YA BUKOBA AIOMBA JAMII KUJENGA UTAMADUNI WA KUWARITHISHA MILA NA DESTURI WATOTO WAO

KATIBU TAWALA WILAYA YA BUKOBA AIOMBA JAMII KUJENGA UTAMADUNI WA KUWARITHISHA MILA NA DESTURI WATOTO WAO

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media - Bukoba

Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba, Bi Proscovia Jaka Mwambi, ameiomba jamii mkoani Kagera kujenga utamaduni wa kuwarithisha watoto wao kujua tamaduni, mila na desturi ili kuwa na maadili mema. 

Mwambi ametoa kauli hiyo akiwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba, Erasto Sima, katika mashindano ya ngoma za asili yaliyofanyika tarehe 26 Julai 2025 katika ukumbi wa Rio De Janeiro, Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera. 

Amesema kuwa kwa sasa watu wameingia na kujikita kwenye masuala ya mitandao ya kijamii zaidi kuliko kuwaelekeza watoto juu ya mila zao, jambo lililosababisha watoto kutokujua mila na tamaduni kutoka kwa wazazi wao

Ameongeza kuwa anatamani mashindano kama hayo ya ngoma A asili yawe makubwa zaidi ili watoto wengi wapate kujifunza mila na desturi.

 Ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa watulivu na kudumisha amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ujao. 

Hata hivyo katibu Tawala huyo, amesisitiza wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kuuweka mji huo katika hali nzuri.

Post a Comment

Previous Post Next Post