" LADIES JOINT FORUM WATAMBULISHA MRADI WA SHE DRIVES TO CHANGE MWANZA.

LADIES JOINT FORUM WATAMBULISHA MRADI WA SHE DRIVES TO CHANGE MWANZA.


 Na Tonny Alphonce, Misalaba Media

Shirika la Ladies Joint Forum la Misungwi Mkoani Mwanza limeutambulisha rasimi mradi wake wa She Drives kwa wadau wenye lengo la  kuwakwamua kiuchumi wanawake na wasichana kutoka kata tatu za wilaya ya Misungwi.

Kupitia mradi huo ambao inatarajiwa kuanza kutekelezwa katika ya mwezi huu wa Saba mwaka huu utawalenga Wanawake na Wasichana 30 wenye umri wa kuanzia miaka 18-35.

Akizungumza na wadau watakaoshirikishwa katika utekelezaji wa mradi huo wilaya Misungwi,Meneja tathimini na ufatiliaji wa shirika la Ladies Joint Forum Mirian Dominick amesema mradi huo utawalenga zaidi wanawake na wasichana waliopitia vitendo vya ukatili wa kijinsia, Wanawake waliozaa wakiwa na umri mdogo,Wanawake wenye ulemavu na Wanawake wanaoishi na Watoto wenye ulemavu.

Mirian amesema mradi huo wa She drives to change utatoa mafunzo Kwa Wanawake na Wasichana uendeshaji wa Bajaji zinazotumia umeme Ili waweze kuingia kwenye biashara ya usafirishaji na kujiongezea kipato Chao binafsi na familia zao.

Kwa upande wake kaimu afisa maendeleo ya Jamii mkoa wa Mwanza Juliana Mwongerezi amelipongeza Shirika la Ladies Joint Forum Kwa kuishirikisha serikali kuhusu mradi huo kuanzia hatua ya awali.

"Hongereni sana Kwa kufuata taratibu zote za uletaji wa mradi katika wilaya ya Misungwi nyinyi mmekuwa tofauti na mashirika mengine ambayo huwa yanaanza utekelezaji wa miradi bila taarifa na wanapokwama huwa ngumu kupata msaada kutoka serikalini".alisema Juliana

Juliana amesema serikali ipo tayari kuhakikisha mradi huo unawalenga wale waliokusudiwa kupitia viongozi wa kata tatu zitakazoguswa na mradi ambazo ni Usagara, Misungwi na Idetemya.

Nao maafisa watendaji kutoka kata za Misungwi,Usagara na Idetemya Vicent Wana, Salome Aron na Magdalena Karoli wamesema wanaupokea mradi huo kwa Kuwa utaenda kubadilisha Maisha ya wananchi wao watakaonufaika na mradi huo.

Mradi wa she drive to change awamu ya pili unaenda kutekelezwa wilayani Misungwi Kwa mwaka mmoja baada ya awamu ya kwanza ya mradi kufanya vizuri katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo zaidi ya Wanawake na Wasichana 2000 walinufaika.

Post a Comment

Previous Post Next Post