" JUMA MWESIGWA AJITOSA UBUNGE KAHAMA MJINI

JUMA MWESIGWA AJITOSA UBUNGE KAHAMA MJINI


Mkurugenzi wa HUHESO Foundation na HUHESO fm - Juma Mwesigwa Mohamed, amejitosa kuomba ridhaa ya chama cha Mapinduzi CCM kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Kahama Mjini kupitia chama hicho.

Mwesigwa amefika ofisi za CCM mapema leo Julai mosi majira ya saa tano asubuhi na kukabidhiwa fomu hiyo na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kahama Andrew chatwanga, ikiwa ni siku ya nne tangu zoezi la uchukuaji wa fomu lilipoanza rasmi ndani ya CCM na linatarajiwa kufikia tamati kesho Julai 2, 2025.




 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post