" MHE. MBONI MHITA AKABIDHIWA OFISI YA MKUU WA MKOA SHINYANGA KUTOKA KWA MHE. ANAMRINGI MACHA

MHE. MBONI MHITA AKABIDHIWA OFISI YA MKUU WA MKOA SHINYANGA KUTOKA KWA MHE. ANAMRINGI MACHA

Mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amepokelewa  rasmi na kukabidhiwa ofisi ya mkuu wa mkoa kutoka kwa mtangulizi wake Mhe. Anamringi Macha ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Akizungumza mara baada ya kupokea ofisi hiyo Mhe. Mboni Mhita ameahidi kusimamia kwa ufanisi utawala bora pamoja na kushughulikia changamoto zilizopo katika mkoa huo huku akilenga kuchochea kasi ya maendeleo kwa ustawi wa wananchi wa Shinyanga.

Amesema kuwa maendeleo ya kweli yanawezekana tu kupitia ushirikiano wa dhati kati ya viongozi wa serikali wananchi na sekta binafsi katika kutekeleza kwa vitendo dhamira ya taifa ya kukuza uchumi na ustawi wa jamii.

Aidha, Mhe. Mhita ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu na kwa amani katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu ujao akisisitiza umuhimu wa kuzingatia katiba na sheria za nchi na kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga amani na utulivu.

Kwa upande wake Mhe. Anamringi Macha ameushukuru uongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha uongozi wake amesema ushirikiano huo umemuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio makubwa na kuwatakia kila la heri katika kipindi kijacho.


Post a Comment

Previous Post Next Post