Na Mwandishi wetu,Mwanza
Bukwimba, Mwanza – Habari njema zimeibuka leo baada ya jina la Philemon Mabuga kuidhinishwa rasmi kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Bukwimba. Hatua hii imepokelewa kwa shangwe kubwa na wakazi wa kata hiyo, ambao wengi wameeleza matumaini makubwa kwa kiongozi huyu kijana mwenye maono ya maendeleo.
Philemon Mabuga amejipatia sifa kwa muda mrefu kutokana na utumishi wake wa kujitolea katika masuala ya kijamii na mipango ya kuinua maisha ya wananchi wa Bukwimba. Wengi wanamuelezea kama kiongozi makini, mwenye maono ya kuhakikisha miundombinu, elimu, afya na ustawi wa wananchi vinaboreka kwa kiwango kikubwa.
Akipokea taarifa ya kuteuliwa kwake, Mabuga aliahidi kuendeleza mshikamano wa wananchi na kuhakikisha kila mwananchi wa Bukwimba ananufaika na fursa zilizopo.
“Hii ni nafasi ya kipekee ya kushirikiana na ninyi wananchi katika kutatua changamoto zinazotukabili na kuinua maendeleo ya kata yetu. Tunaenda kushirikiana bega kwa bega kwa mshikamano na mshirikiano wa kweli,” alisema Mabuga.
Wananchi wengi wameahidi kumuunga mkono kwa kishindo, wakieleza kuwa Mabuga anaonesha dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya yanayogusa maisha ya kila mmoja.

Post a Comment