" MADEREVA MKOANI KAGERA WATAKIWA KUZINGATIA MATENGENEZO YA MAGARI KATIKA GEREJI ZA SERIKALI

MADEREVA MKOANI KAGERA WATAKIWA KUZINGATIA MATENGENEZO YA MAGARI KATIKA GEREJI ZA SERIKALI

Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaMadereva mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia na kukagua magari yao kwa kuyapeleka matengenezo katika gereji zilizoelekezwa na serikali, ikiwemo Temesa, na si kuyapeleka katika garage zisizo rasmi zinazojulikana kama "garage za chini ya mwembe."Kauli hiyo imetolewa na kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania mkoani Kagera, Mhandisi Prisca Mazigo, wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake. Mhandisi Mazigo amesema kwamba madreva wanatakiwa kuepuka kutengeneza magari yao nje ya garage zisizo rasmi, kwani wengi wamekuwa wakipeleka magari yao katika gereji ambazo hazieleweki na kusababisha madhara makubwa kwa magari hayo. Amesema kuwa, gereji za watu binafsi zina changamoto nyingi ambapo mara nyingi wahandisi wanajitahidi kuonyesha kuwa wanamrahisishia mteja gharama kwa kutengeneza sehemu chache, lakini wanaweza kuweka vifaa visivyo sahihi na kutumia mafuta duni.Ameongeza kuwa hali hiyo inaathiri hali ya gari, na hatimaye mteja anaweza kujikuta ameharibu gari lake bila kujua."Baada ya gari kurudishwa kutoka Temesa baada ya kutengenezwa kwenye garage za chini ya mwembe, mara nyingi inakuwa na matatizo zaidi ya 50 na haiwezi kutengenezwa tena; tayari imeshaharibika bila taarifa," alisema Mhandisi Mazigo.Hata hivyo amewaomba madereva kuwa makini na kutosita kwenda Temesa, ambayo ni sehemu sahihi ya matengenezo ya magari, kama ilivyoelekezwa na serikali katika sheria ya manunuzi.Amewasisitiza viongozi wa Serikali na waajiri wa magari kwamba ni muhimu kupeleka magari Temesa kwa ajili ya matengenezo. Mhandisi Mazigo pia amewapongeza madreva ambao wanatekeleza utaratibu wa serikali kwa kupeleka magari yao Temesa kwa ajili ya matengenezo sahihi.Kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania mkoani Kagera, Mhandisi Prisca Mazigo

 

Post a Comment

Previous Post Next Post