" MFUMO WA KUWATAMBUA WAKULIMA WAZINDULIWA.

MFUMO WA KUWATAMBUA WAKULIMA WAZINDULIWA.


Na: Belnardo Costantine.

Wizara ya kilimo kupitia waziri wa wake  Hussein Bashe Imezindua Kampeni ya ya kumtambua mkulima na kurahisisha mawasiliano baina ya mkulima na maafisa ugani yenye jina la Mali Shambani.

waziri  Bashe amesema  kuwa mfumo huo  utarahisisha  mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wakulima na wataalamu wa kilimo kwa lengo la kuboresha sekta ya kilimo.

Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Umahiri cha mazao kilichopo Mtanana, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma leo Julai 16, 2025 na kushirikisha wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima.

"Tunataka tuwe na ‘direct communication’ (Mawasiliano ya moja kwa moja) na wakulima sisi wizara ya kilimo. Kwa hiyo tunatumia njia mbalimbali rasmi kwa sababu tunafanya kazi na Halmashauri lakini majadiliano na wakulima moja kwa moja na wataalamu wa wizara ya kilimo kule vijijini ndio programu hii inakwenda na itakuwa programu ya mwaka mzima kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu"
Amesema waziri Bashe .

hata hivyo ameongeza   kuwa  mfumo huo wa wa kidigitali wa ugani ni mfumo ambao wakulima wote watakuwa nao kwenye simu zao.

"  mkumbuke tulianza na usajili wa wakulima kama miaka miwili, mitatu iliyopita na sasa hivi tumefika jumla ya wakulima karibu milioni nne na kidogo, lengo letu ni kusajili wakulima milioni saba"

Amesema Bashe .

Aidha Waziri Bashe amesema tayari wakulima wameanza kupatiwa hati za mashamba yao ili kuwaingiza katika mfumo rasmi na kwamba sasa Maafisa ugani waliothibitishwa nao wanaanza kusajiliwa katika mfumo ambao mkulima atakuwa nao kwenye simu yake kwa lengo la kumtambua Afisa ugani aliyethibitishwa na Serikali lengo likiwa ni kuwaondoa wababaishaji  " Vishoka" kwenye sekta ya kilimo.
 wakulima wameipongeza hatua hiyo ya serikali na kusema kuwa itawarahishia kupata huduma kwa haraka ikiwemo upatikanaji wa masoko na pia kuongeza tija katika kilimo chao kupitia teknolojia ya kilimo kiganjani ambayo pia Waziri Bashe aliizindua.

Post a Comment

Previous Post Next Post