
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwezeshaji
maarufu na Mkurugenzi wa The True Life Foundation, Peter Frank maarufu kama Mr. Black, ameanza
ziara yenye jina la Tanzania School to School Tour chini ya mradi wa Youth
Perspective Forum unaoendeshwa na The BSL Investment Co. Ltd wakishirikiana na The True
Life Foundation.
Ziara hiyo
inalenga kutoa mafunzo kwa vijana, taasisi mbalimbali, na
watumishi wa vyuo na shule za sekondari na msingi Tanzania, kwa
lengo la kuwawezesha kijamii, kitaaluma na kiutu, kupitia mafunzo ya moja kwa
moja katika maeneo yao ya kujifunzia.
Mafunzo ya awamu
ya kwanza yanaanza leo Ijumaa, Julai 25, 2025, katika Chuo cha City College – Mwanza Campus, kuanzia saa 4:00
asubuhi hadi saa 10:00 jioni, yakihusisha wanafunzi wa elimu ya juu waliopo
chuoni hapo na maeneo ya jirani.
Kesho, Jumamosi
Julai 26, Mr. Black ataendelea na awamu ya pili ya ziara hiyo katika Inspire Science School iliyopo Kibaha,
mkoani Pwani, ambapo mafunzo yataanza saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana.
Mada
mbalimbali zitakazofundishwa katika ziara hii ni pamoja na:
1. Ujenzi wa Timu (Team Building)
2. Huduma kwa Wateja (Customer Care)
3. Uwasilishaji wa Maudhui na Tabia Bora
4. Masoko, Uuzaji na Uwekaji Chapa
5. Maadili, Tathmini na Uhakiki
6. Michezo ya Kiingereza na Matamshi Sahihi
Mr. Black
ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya BSL Investment Co. Ltd, amesema mafunzo hayo yamelenga
kusaidia vijana kutambua nafasi yao katika jamii, kukuza ubunifu na kuwaandaa
kwa ushindani wa soko la ajira.
Kwa maelezo zaidi au kushiriki katika ziara zijazo,
wasiliana kupitia:
📞 0712 583 756 / 0752 849 726
📧 pblack969@gmail.com
📱 Instagram: @bslschools
Post a Comment