Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga SC wamemtambulisha rasmi Romain Folz kuwa Kocha wao Mkuu mpya akichukua nafasi ya Miloud Hamdi.
Wasifu wa Romain Folz kwa ufupi
Ana umri wa miaka 34 akiwa amezaliwa Juni 28 mwaka 1990
Raia wa Ufaransa
Mfumo anaopendelea ni 4-3-3 wakiwa wanazuia (Kwa mujibu wa Transfermarket)
Kazi zake za nyuma
Golden Eagles (Kocha Msaidizi kuanzia 1 Julai 2017 mpaka Juni 30 2017)
West Virginia (Kocha Mkuu kuanzia 6 Januari 2018 mpaka 6 Januari 2019)
Uganda NT (Kocha Msaidizi wa Sebastian Desabre kuanzia 6 Januari 2019 mpaka 6 Julai 2019)
Pyramids (Kocha Msaidizi wa Sebastian Desabre kuanzia 1 Agosti 2019 mpaka 1 Januari 2020)
Bechem United (Kocha Mkuu kuanzia 20 Januari 2020 mpaka 20 Julai 2020)
Chamois Niort (Kocha Msaidizi Sebastian Desbare kuanzia 20 Julai 2020 mpaka 27 Machi 2021)
Ashanti Gold (Kocha Mkuu kuanzia 28 Machi 2021 mpaka 10 Mei 2021).
Mauritania (Kocha Msaidizi wa Corentin Martins, Didier Gomes na Gerard Buscher kuanzia 1 Juni 2021 mpaka 9 Disemba 2021)
Township Rollers (Kocha Mkuu kuanzia 10 Disemba 2021 mpaka 30 Juni 2022)
Marumo Gallants (Kocha Mkuu kuanzia 1 Julai 2022 mpaka 4 Septemba 2022)
Amazulu Fc (Kocha Mkuu kuanzia 9 Oktoba 2022 mpaka 5 Aprili 2023)
Amazulu (Mkurugenzi wa Michezo kuanzia 5 Aprili 2023 mpaka 30 Juni 2023)
Horoya Fc (Kocha Mkuu kuanzia 10 Agosti 2023 mpaka 10 Oktoba 2023)
Mtathmini wa viwango wa FIFA kuanzia 10 Novemba 2023 mpaka 9 Julai 2024).
Mamelodi Sundowns (Kocha Msaidizi wa Manqoba Mngqithi na Miguel Cardoso kuanzia 10 Julai 2024 mpaka 10 Februari 2025)
Olympique Akbou (Kocha Mkurugenzi wa Michezo kuanzia 14 Machi 2025 mpaka 13 Julai 2025)
Post a Comment