Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Mwenyekiti wa Soko la Kimataifa la Madini Mkoani Mwanza, William Kulindwa alipongeza dhamira ya serikali kuanzisha masoko ya madini hapa nchini kwani hali hiyo imechochea kukua kwa sekta Mkoani Mwanza.
Alisema wachimbaji wadogo vilevile wameweza kupata sehemu ya kuuzia madini yao kwa bei nzuri kwani kwa sasa eneo hilo lina makampuni 30 ya kununua madini ya dhahabu, Silver na kampuni moja inanunua germstone.
Meneja wa Kampuni ya Ngemba Mining, Calvin Thobias alipongeza kuwepo kwa ulinzi na usalama unaowawezesha kufanya shughuli zao kwa amani bila bughudha yoyote.
Alisema vilevile kuwepo kwa midahalo inayofanywa mara kwa mara na Wizara ya Madini ambapo husikilizwa kero zinazowakabili kuwa hatua nzuri wanayofurahia.
Meneja wa Kampuni ya Fregom Ltd, Dominic Mogore alisema soko linawezesha madini kununuliwa kwa bei nzuri huku michakato mingi ya leaching, elution, refining na mingine imetoa wigo mpana kwa ajira.
Halima Mwita, mfanyakazi wa Fregom alisema anashikuru kupata ajira ambayo inamufanya ajiandae kwa ajili ya masomo yake huku akiwaomba vijana wenzake me uchangamkia fursa za madini.
Post a Comment