" WAZIRI AWESO AIPONGEZA CCM MKOA WA KAGERA

WAZIRI AWESO AIPONGEZA CCM MKOA WA KAGERA


Na Lydia Lugakila, Misalaba Media

Waziri wa maji Jumaa Aweso amekishukuru chama cha mapinduzi (CCM) Mkoani Kagera kutokana na kufanya kazi usiku na mchana na kuhakikisha mambo yanaenda vizuri 

Waziri Aweso ametoa kauli hiyo alipotembelea ofisi za chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Kagera akiwa katika ziara maalum ya kukagua miradi ya kimkakati ya miji 28 na kuwakumbusha wakandarasi wanaopewa kazi na kumaliza kwa wakati.

Amesema kuwa wizara hiyo haitakuwa sehemu ya kupunguza kura za chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao bali watakuwa sehemu ya kuongeza kura za chama hicho ili kuhakikisha yale yaliyoahidiwa yanatekelezwa.

Aidha amewahimiza viongozi mkoani humo kufanya kazi kwa kukishirikisha na chama hicho ili waweze kufanikiwa ipasavyo.

"Ndugu zangu msiwe katika chama cha mapinduzi kiujanja janja bali muwe nacho katika kupanga na kushauriana," alisema Waziri Aweso.

Ameongeza kuwa malengo yao ni kuhakikisha ifikapo Desemba 2025 wawe na asilimia 85 ya upatikanaji wa maji vijijini na asilimia 95 upatikanaji wa maji mjini.

Hata hivyo amesema kuwa chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kilichomlea hivyo ni lazima akitumikie kwa nguvu zote.

Post a Comment

Previous Post Next Post