" WADAU WA MADINI WAFUNGUKA YALIYOFANYIKA MWANZA

WADAU WA MADINI WAFUNGUKA YALIYOFANYIKA MWANZA


Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

WADAU wa sekta ya madini katika Soko Kuu la Kimataifa la Madini Mkoani Mwanza wamepongeza kupatikana kwa ufanisi wenye tija uliowezesha kuongezeka kwa makusanyo hadi bilioni 12 kwa mwaka 2024/25 na kuzalisha ajira kwa vijana wa kitanzania.

Hayo yamebainishwa Leo jijini mwanza 25/7/2025/ Pansiansi Wilaya ya Ilemela Mkoani mwanza nyakati tofauti kwenye soko hilo walipokuwa wakizungumza na Misalaba Media kuhusiana mwenendo wa sekta ya madini katika miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.

Mchambuzi Fedha Mwandamizi wa Ofisi ya Madini Mkoani Mwanza, Elinami Kimaro alisema awali walikuwa wakikusanya bilioni 7 miaka ya 2021/22 hivyo kutokana usimamizi mzuri na ushirikishwaji kumekuwepo na ongezeko.

Alisema wametoa leseni 661 kwa wachimbaji wadogo mwaka 20/25 tofauti na miaka ya nyuma ambapo mwaka 2020/21 walitoa 250 hali hiyo ikitokana na sera nzuri za kodi.

Mwenyekiti wa Soko la Kimataifa la Madini Mkoani Mwanza, William Kulindwa alipongeza dhamira ya serikali kuanzisha masoko ya madini hapa nchini kwani hali hiyo imechochea kukua kwa sekta Mkoani Mwanza.

Alisema wachimbaji wadogo vilevile wameweza kupata sehemu ya kuuzia madini yao kwa bei nzuri kwani kwa sasa eneo hilo lina makampuni 30 ya kununua madini ya dhahabu, Silver na kampuni moja inanunua germstone.

Meneja wa Kampuni ya Ngemba Mining, Calvin Thobias alipongeza kuwepo kwa ulinzi na usalama unaowawezesha kufanya shughuli zao kwa amani bila bughudha yoyote.

Alisema vilevile kuwepo kwa midahalo inayofanywa mara kwa mara na Wizara ya Madini ambapo husikilizwa kero zinazowakabili kuwa hatua nzuri wanayofurahia.

Meneja wa Kampuni ya Fregom Ltd, Dominic Mogore alisema soko linawezesha madini kununuliwa kwa bei nzuri huku michakato mingi ya leaching, elution, refining na mingine imetoa wigo mpana kwa ajira.

Halima Mwita, mfanyakazi wa Fregom alisema anashikuru kupata ajira ambayo inamufanya ajiandae kwa ajili ya masomo yake huku akiwaomba vijana wenzake me uchangamkia fursa za madini.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post