" PETER ALEX FRANK (MR. BLACK) AUTAKA UDIWANI KATA YA KIZUMBI

PETER ALEX FRANK (MR. BLACK) AUTAKA UDIWANI KATA YA KIZUMBI


NA Mapuli Kitina Misalaba 

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Peter Alex Frank maarufu kwa jina la Mr. Black, amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho ili kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.

Mr. Black ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi na Vijana Wilaya ya Shinyanga Mjini, pia ni Mjumbe wa Baraza la Vijana wa CCM. Mbali na shughuli za kisiasa, yeye ni mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya The BSL Investments Company Limited pamoja na shule za BSL Schools zilizopo Tanzania na Rwanda.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu, Peter Alex Frank amesema amejipanga kuipeleka Kata ya Kizumbi katika ramani ya dunia kupitia ubunifu, ushirikishwaji wa jamii, na msukumo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku akisisitiza kuzingatia misingi ya utawala bora.

Ametumia nafasi hiyo pia kupongeza juhudi za Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuijenga Tanzania mpya yenye dira ya maendeleo endelevu.

Post a Comment

Previous Post Next Post