
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa SACP Shadrack Masija wakati alizungumza na waandishi wa habari
………………
Na Neema Mtuka Nkasi
Rukwa :Jeshi la polisi mkoa wa Rukwa limewakamata wanachama 11 wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kati yao wanaume Saba na wanawake 4 wakiwemo viongozi wanne wa chama hicho kwa kufanya mkusanyiko usio halali.
Akizungumza leo Julai 28 ,2025 kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi SACP Shadrack Masija amewataja wanachama hao pamoja na viongozi waliokamatwa.
Viongozi hao ni Winifrida Joseph Khenani (Katibu Mwenezi wa baraza la vijana jimbo la Nkasi kaskazini) Godfrid Bendera (Katibu wa Chadema Jimbo la Nkasi kaskazini) Evarist Mwanisawa (Katibu baraza la wazee chadema wilaya ya Nkasi )na Scolastica Mwalonde (Mwenyekiti wa chadema kata ya majengo).
Jeshi la polisi mkoa wa Rukwa linawataka mhe.Aida Khenani mbunge wa jimbo la Nkasi kaskazini) na Albeto John Kaliko maarufu kama Galincha (aliyekuwa diwani wa kata ya Itete) kujisalimisha polisi wilaya ya Nkasi au ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Rukwa kwa kupanga mkusanyiko huo usio halali.
Kamanda Masija amesema kufuatia kukamatwa wanachama hao wa (CHADEMA),kumeibuka watu wanaotuma taarifa za uongo ,upotoshaji na za kubuni kwenye mitandao ya kijamii wakiwa na lengo la kuitia hofu Jamii ya watanzania au kulichonganisha jeshi la polisi na wananchi.
Hivyo jeshi la polisi mkoa wa Rukwa linamtaka mtu mmoja aitwaye Alfred Sotoka kuripoti ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Rukwa kufuatia kutuma taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na tukio hilo.
Ninamtaka Sotoka kujisalimisha wala usijifiche kwani utasakwa popote ulipo”amesema kamanda
Aidha kamanda Masija amewataka wananchi kufuata sheria wanapotaka kufanya mkusanyiko.
Pia amesema wananchi wanatakiwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii na ya mawasiliano kwa kuacha tabia za kutoa au kusambaza taarifa wasizo na uhakika nazo .
Post a Comment