Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa, iliyoketi leo Jumatatu,tarehe 28 Julai 2025, Dodoma, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wametoka kikaoni, baada ya kikao hicho kumalizika usiku huu.
Wakati wowote kuanzia sasa, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla, atazungumza na waandishi wa habari wa kitaifa na kimataifa, katika Ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM, Dodoma.
Post a Comment