" Serikali Yatangaza Bei Mpya ya Gharama za Kupima DNA

Serikali Yatangaza Bei Mpya ya Gharama za Kupima DNA

 

Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali haina lengo la kupata faida kwa shughuli zake, bali inatoa huduma kwa wananchi kwa gharama nafuu, amesema Dkt. Fidelice Mafumiko, Mkemia Mkuu wa Serikali.

Akizungumza na vyombo vya habari, Dkt. Mafumiko alifafanua kuwa gharama ya shilingi laki moja inayotozwa kwa kila sampuli inayochukuliwa ni ndogo mno ukilinganisha na gharama halisi ya uchunguzi huo.

Alisema kuwa Serikali ndiyo inayobeba sehemu kubwa ya gharama hizo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bila vikwazo vya kifedha.

“Maabara ya Mkemia Mkuu haifanyi biashara bali tunatoa huduma muhimu kwa jamii. Lengo letu si kutengeneza faida, bali kusaidia mfumo wa haki, afya na usalama wa jamii.

Hii ndiyo maana gharama ya shilingi laki moja ni ya chini mno ikilinganishwa na gharama halisi ya mchakato mzima,” alisema Dkt. Mafumiko.

Ameongeza kuwa juhudi za serikali katika kugharamia huduma hizi ni sehemu ya dhamira yake ya kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati kupitia ushahidi wa kisayansi unaotolewa na maabara hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post