" UCHAGUZI WA MADIWANI WA VITI MAALUM UWT WAFANYIKA KWA AMANI KATIKA TARAFA ZA MANISPAA YA SHINYANGA

UCHAGUZI WA MADIWANI WA VITI MAALUM UWT WAFANYIKA KWA AMANI KATIKA TARAFA ZA MANISPAA YA SHINYANGA

 Na Mapuli Kitina Misalaba

Zoezi la upigaji kura za maoni za Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) kwa ajili ya kupata wagombea wa nafasi za udiwani wa viti maalum CCM katika Manispaa ya Shinyanga limekamilika kwa amani katika tarafa zote tatu za Mjini, Ibadakuli na Old Shinyanga.

Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Bi. Salama A. Mhampi, amesema zoezi hilo limefanyika kwa kufuata kanuni na taratibu zote za chama huku wanawake wakijitokeza kwa wingi kugombea na kupiga kura.

Katika Tarafa ya Mjini, Moshi Hussein Kanji ameibuka mshindi kwa kupata kura 536, akifuatiwa na Ester Festo Makune aliyepata kura 444, na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Veronica E. Massawe aliyepata kura 431. Pia Mwanahamis Kazoba amepata kura 355 huku Eunice Manumbu akipata kura 272. Jumla ya wagombea 18 walishiriki katika uchaguzi huo wa tarafa ya Mjini.

Kwa upande wa Tarafa ya Ibadakuli, Zuhura Waziri Mwambishi ameshinda kwa kishindo baada ya kupata kura 695, akifuatiwa kwa mbali na Anascholastica Methew Maige aliyepata kura 59, huku Angelina Deus Kaza akijipatia kura 4 pekee.

Naye katika Tarafa ya Old Shinyanga, Mwanaidi Abdul Sued ameongoza kwa kura 539, akifuatiwa na Picca Nuhu Chogero aliyepata kura 187, na Lilian  Nyagetera akamaliza wa tatu kwa kura 27.

Zoezi hilo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, ambapo UWT kama ilivyo kwa jumuiya nyingine za CCM, inafanya kura za maoni kuwachagua wagombea wake.

Post a Comment

Previous Post Next Post