" WADAU WA MADINI MWANZA WAIPONGEZA SERIKALI KUWEZESHA MAKUSANYO YA BIL12

WADAU WA MADINI MWANZA WAIPONGEZA SERIKALI KUWEZESHA MAKUSANYO YA BIL12

 

Mchambuzi wa Fedha Mwandamizi wa Ofisi ya Madini Mkoani Mwanza, Elinami Kimaro

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

WADAU wa sekta ya madini katika Soko Kuu la Kimataifa la Madini Mkoani Mwanza wamepongeza kupatikana kwa ufanisi wenye tija uliowezesha kuongezeka kwa makusanyo hadi bilioni 12 kwa mwaka 2024/25 na kuzalisha ajira kwa vijana wa kitanzania.

Hayo yamebainishwa jijini hapa jana kwa nyakati tofauti na wadau  kwenye soko hilo walipokuwa wakizungumza na Mwandishi wetu kuhusiana na mwenendo wa sekta ya madini katika miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.

Mchambuzi wa Fedha Mwandamizi wa Ofisi ya Madini Mkoani Mwanza, Elinami Kimaro alisema awali walikuwa wakikusanya bilioni 7 miaka ya 2021/22 hivyo kutokana usimamizi mzuri na ushirikishwaji kumekuwepo na ongezeko.

Alisema wametoa leseni 661 kwa wachimbaji wadogo mwaka 20/25 tofauti na miaka ya nyuma ambapo mwaka 2020/21 walitoa 250 hali hiyo ikitokana na sera

Post a Comment

Previous Post Next Post