Hayo yamebainishwa hivi karibuni na wadau wa Sekta ya madini mkoani Geita walipokuwa wakichangia mafanikio yaliyofikiwa kwenye eneo hilo tangia awamu ya sita ilivyoanza jitihada zake
“Tunashukuru kuwepo kwa maendeleo katika Sekta ya madini hapa mkoani Geita ambapo ni kitovu cha madini” alisema Nshoma
Alisema kuwepo kwa maendeleo katika Sekta hiyo kunatokana na uwepo kwa Nishati ya uhakika pamoja na sera Nzuri zilizochochea Sekta hiyo hapa nchini.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa chama cha ushirika mgusu miners ambao ni chama cha ushirika wa Mkoani Geita Nshoma alisema anashukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuleta maboresho yaliyopelekea kuanzishwa kwa Masoko ya madini hapa mkoani Geita.
Alisema hatua hiyo imesaidia kuongeza thamani kwa madini yanayochimbwa katika Mkoa huo kwani imewezesha kuwepo kwa ushindani katika ununuzi wa madini hayo hivyo kuongezea thamani yake.
“Tunaishukuru serikali kwa kufungua milango ya uwekezaji kwenye Sekta ya madini kwani hali hiyo imetufanya tujiendeshe kwa faida huku kampuni yetu ikiajiri Vijana” alisema Nshoma
Nshoma alisema kuwa vilevile wachimbaji wameongezeka katika Maeneo tofauti ndani ya Mkoa huo ambapo Vijana wa kitanzania waweza kujiajiri katika uchimbaji wa madini huku wakitumia telnolojia za kisasa katika uendeshaji wa kazi.
Post a Comment