" WAGANGA WA TIBA ASILI KUNOLEWA MWANZA

WAGANGA WA TIBA ASILI KUNOLEWA MWANZA

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

KATIBU Mkuu wa Chama cha Waganga Tameso (T) Tanzania, Lukasi Mlipu amefanya ziara Mkoani Mwanza kuhamasisha Waganga wa Tiba Asili katika eneo hilo kushiriki kwenye wiki ya Tiba Asili itakayofanyika kitaifa mkoani Dodoma.

Akizungumza 23/7 /2025 .Jijini Mwanza katika Eneo la Mwalo wa Igombe wilayani Ilemela Mkoani Mwanza aliwataka Waganga wa Tiba Asili wote kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuhudhuria tukio hilo muhimu ambalo sambamba na kutowa elimu wataweza kutoa usajiri kwa ambao hawajasajiliwa.

Mlipu amesema wao kama chama wamejipanga kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya kiharifu vya watu wasio na Leseni maarufu Kama makatauzinga ambao wamekuwa wakiendelea kujenga wasiwasi kwa watu hapa nchini.

Naye Mkuu wa Polisi Jamii wilaya ya Ilemela Doloph mghenyi amempongeza katibu mkuu wa Chama hicho kwa kutoa elimu na kuhamasisha kutojihusisha na ramli chonganishi.

"Tunaomba ndugu zangu waganga wa tiba asili jitokezeni kwenye mkutano wetu Dodoma"alisema Mulipu.

Mghenyi aliwataka wananchi  kutoa taarifa pindi wanapoona matendo yasiyo rasmi yanayoweza kuvuruga amani kutokana na tiba za waganga wa tiba asili.

Post a Comment

Previous Post Next Post