Na Lydia Lugakila, Bukoba
Jamii ya Khoja Shia Ithnaasheria imewaomba wananchi Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera kujitokeza na kushiriki kwa wingi katika zoezi maalum la kuchangia damu linalotarajiwa kufanyika julai 5 2025.
Kwa mujibu mwenyekiti wa Taasisi ya Khoja Shia Ithnaasheria Murtazza Visram zoezi hilo linalenga kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji mkubwa wa damu hospitalini, katika kuadhimisha Siku ya Imam Hussein.
Aidha Visram ameongeza kubwa zoezi hilo litafanyika katika Msikiti wa Khoja Shia Ithnaasheria, uliopo Manispaa Bukoba katika eneo la Jaffery Schools.
Wandaaji wa zoezi hilo wamesema kuwa kuchangia damu ni kitendo muhimu kinachoweza kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji, wa ajali na uzazi, pamoja na kutoa matumaini kwa wale walio hospitalini kwa dharura.
Wameongeza kuwa Huduma zote zitafanyika kwa uangalizi wa kitabibu na kwa usalama wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wachangiaji wanapata huduma bora.
Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, RED CROSS kitaweka wawakilishi katika tukio hili, kusisitiza umuhimu wa kuchangia damu, kama sehemu ya maisha yako kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine.
Hata hivyo wananchi wameelekezwa kuwasiliana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Khoja Shia, Murtazza Visram ili kufanikisha zoezi hilo kwa haraka.
Huu ni wito wa dharura kwa jamii kuungana na kusaidia kuokoa maisha ya wengine katika kipindi hiki cha mahitaji makubwa.
Post a Comment