
Na Mapuli Kitina Misalaba
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eunice Jackson Wiswa, leo Jumanne Julai 1, 2025 amejiorodhesha rasmi kuwania ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Eunice ambaye ni mtaalamu wa Jiolojia na mwenye uzoefu mkubwa kwenye sekta ya Madini, Mafuta na Gesi, ameonesha dhamira ya dhati ya kulitumikia jimbo hilo, akisema anayo nia, uwezo na uzoefu wa kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga Mjini.
Hii si mara yake ya kwanza kuonesha nia ya kugombea nafasi hiyo, kwani mwaka 2020 pia alijitokeza kuomba ridhaa ya chama hicho tawala kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo.
Hatua ya Eunice kuingia tena kwenye kinyang’anyiro hicho ni ishara ya kuendelea kuweka mbele maslahi ya wananchi wa Shinyanga Mjini na kuonyesha kuwa yupo tayari kusimamia ajenda za maendeleo kwa weledi na uwajibikaji mkubwa.
Kwa sasa, mchakato wa uchukuaji wa fomu ndani ya CCM unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, huku wagombea mbalimbali wakiendelea kujitokeza kuwania nafasi za udiwani na ubunge.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment