Na Mapuli Kitina Misalaba
Mfanyabiashara maarufu na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gilitu Makula, leo Juni 28, 2025, amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama hicho tawala.
Makula amechukua fomu hiyo katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, hatua inayodhihirisha dhamira yake ya kutaka kulitumikia jimbo hilo kwa nafasi ya ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Hii ni miongoni mwa hatua za mwanzo katika mchakato wa ndani ya chama hicho ambapo wanachama mbalimbali wanaendelea kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwa ni pamoja na ubunge, udiwani na urais.
Post a Comment