" MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI MHE. JAJI MWAMBEGELE AKAGUA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA MAGEREZANI KAGERA NA GEITA

MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI MHE. JAJI MWAMBEGELE AKAGUA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA MAGEREZANI KAGERA NA GEITA

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Juni 28, 2025 ametembelea na kukagua mwenendo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Magereza ya Bukoba, Muleba, Biharamulo mkoani Kagera na Chato mkoani Geita. Mzunguko wa tatu wa awamu ya pili ya uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Wafungwa chini ya miezi sita na mahabusu waliopo katika Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo Zanzibar umeanza leo Juni 28, 2025 na utaendelea kwa siku saba hadi Julai 04, 2025.

Post a Comment

Previous Post Next Post