Mkuu wa Mkoa Arusha Kenan Kihongosi akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa Manyara Queen Sendiga leo katika viwanja vya Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Mkoani Manyara
Na, Egidia Vedasto - Misalaba Media, Arusha.
Wananchi Mkoani Arusha wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura pindi wakati utakapowadia ili wapate viongozi watakaoleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika Taifa letu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa Manyara Queen Sendiga baada ya kumaliza mzunguko wa Mkoa mzima, Mkuu wa Mkoa Arusha Kenan Kihongosi amehimiza amani na utulivu wakati wa uchaguzi, kwa maana ya kwamba kila baada ya mtu kupiga kura anatakiwa akatulie nyumbani kusubiri matokeo.
"Nawasihi wananchi wenzangu kama kauli mbiu ya mwenge inavosema tujitokeze kwa wingi katika uchaguzi mkuu, ili kupiga kura kwa haki na aman,na nina waahidi kuwa Serikali tumejinga kikamilifu kuhakikisha tunakabiliana na changamoto yeyote ile itakayojitokeza kukwamisha zoezi hilo"amesisitiza Kihongosi.
Hata hivyo ameongeza kuwa, kwa siku saba ambazo Mwenge umekimbizwa Mkoani humo, umezindua, kuweka jiwe la msingi pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo ya afya,miundombinu,elimu na maji.Sambamba na hayo, Mwenge wa Uhuru ulipokuwa Wilayani Arusha ulikagua miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 8.
Hata hivyo katika sekta ya afya, licha ya kuzindua mashine ya saratani ya matiti pia wananchi wameweza kupatiwa huduma mbalimbali za kiafya vipimo na matibabu.
"Kwa upande wa UKIMWI Arusha mjini wamepimwa wagonjwa 2570 na kati yao nane ndio wamekutwa na maambuzi ya UKIMWI, wamepewa ushauri nasaha na kupatiwa elimu juu ya kuzingatia lishe bora"Amefafanua Kihongosi.
Akipokea mwenge huo Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ameahidi kuwa Mwenge utakapokuwa Mkoani kwake, utafanya shughuli zote zilizokusudiwa hadi hapo utakapokabidhiwa katika Mkoa wa Singida kwa ajili ya kuendelea na ratiba zingine.
Katika namna hiyohiyo Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa,Ismail Ali Ussi aliumwagia Sifa Mkoa wa Arusha na kusema kuwa katika mikoa waliokwisha itembelea hadi sasa, Arusha umekuwa mkoa wa Kutolewa mfano.
“Nakupongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Arusha,wewe pamoja na kamati yako kwani hadi sasa tumeishatembea katika mikoa 17 ila Mkoa wa Arusha umeonyesha mfano wa kuigwa katika kusimamia mirdi ya maendeleo na kwa maana hiyo hadi kufikia sasa nyie ndo mnaongoza”amesema.
Pamoja na hayo ameitaka Mikoa mingine kuiga mfano Mkoa wa Arusha ,kwa kusismamia vema fedha zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo kwa kuepuka ubadhirifu na kuhakikisha miradi inatekelezwa na kukamilika kwa kiwango kinachotakiwa.
Post a Comment