Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema ni nafasi ya watanzania sasa kupambana kwaajili ya haki, uhuru na maisha bora mwa watoto wa Kitanzania wa sasa na wa baadae, akisisitiza kuwa Oktoba 2025 ni fursa ya kuleta mabadiliko kwa Watanzania.
“Maamuzi ya busara ya Tanu mwaka 1958 yalituletea uhuru. Maamuzi ya busara ya ACT Wazalendo kushiriki uchaguzi wa mwaka 2025 yatatuletea maisha bora na hii tunapaswa tujikumbushe roho ya maji Maji- Umoja, nguvu na mapambano. Tushiriki, tupige kura na tuiondoe CCM” amesema Zitto Kabwe.
Zitto amebainisha hayo wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Uyui Sekondari Mjini Tabora, akihimiza wananchi kushiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wakiwa na dhamira moja ya kulinda kura zao kwa nguvu zote.
Zitto kadhalika amebainisha kuwa miaka mitano ya Bunge la CCM peke yake imetosha na kwamba miaka mingine mitano ya Bunge la namna hiyo haliwezekani na kwamba ACT Wazalendo inaenda kurejesha heshima ya Bunge la Tanzania
Akizungumzia hali ya kiuchumi, Zitto amesema Chama hicho kinapambana dhidi ya dhulma ya kiuchumi inayosababishwa na sera dhaifu za CCM ambazo amedai kuwa zimeifanya Tabora pamoja na mikoa Mingine ya Kigoma, Katavi, Rukwa, Kagera, Shinyanga, Geita na Simiyu kuwe ukanda wa umaskini nchini.
Amesema hali hiyo imetokana matokeo ya sera za CCM ambazo zimepuuza maendeleo ya Vijijini na kushindwa kusaidia sekta ya kilimo ambayo ni moyo wa maisha ya theluthi mbili ya watanzania ikiwa inachangia theluthi moja tu ya pato la Taifa
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment