Abiria wanaosafiri safari za usiku kwa kutumia mabasi wamepewa elimu ya usalama barabarani ikiwemo onyo dhidi ya tabia ya kutoka kwenye viti vyao na kulala chini kwenye njia ya kupita abiria ndani ya basi.
Elimu hiyo imetolewa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, mara baada ya kubainika kuwa baadhi ya abiria wanapopatwa na usingizi nyakati za usiku huamua kulala sakafuni hali inayohatarisha usalama wao.
Sajenti Ndimila amesema kitendo hicho kinaweza kusababisha madhara makubwa pale gari linapopata mtikisiko wa ghafla, ambapo abiria wanaolala chini hujikuta wakipiga kelele au kujigonga na kuumia sehemu mbalimbali za mwili hususani kichwani.
Amefafanua kuwa kwa usalama wa maisha yao, abiria wanapaswa kukaa kwenye viti vyao muda wote wa safari na kufunga mikanda mpaka wanapofika safari zao. Ameongeza kuwa hatua hiyo siyo tu inalinda maisha yao binafsi bali pia inapunguza changamoto za uokoaji endapo ajali itatokea.
Aidha, ameendelea kuwasisitiza abiria wote kuwa walinzi wa afya na maisha yao kwa kufuata maelekezo ya usalama barabarani, huku akitoa rai ya kila mmoja kushirikiana katika kuhakikisha safari zote za usiku na mchana zinakuwa salama bila madhara yanayoweza kuepukika.

GUSA LINK HAPA CHINI👇
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment