
Zoezi la uokoaji katika machimbo ya Nyandolwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga limeendelea leo kwa mafanikio, baada ya miili ya wachimbaji wawili kutolewa kutoka chini ya mgodi wa Kikundi cha Wachapakazi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amesema miili hiyo imetolewa kutoka duara namba 20C na kutambulika kuwa ni Japhet Masanja (30), mkazi wa Lunguya Kahama na Chembanya Makenzi (25), mkazi wa Nyandolwa Shinyanga.
Amesema kufuatia hatua hiyo, idadi ya watu waliotolewa kufikia sasa ni 10, huku wachimbaji 15 wakiendelea kufukiwa ardhini.
“Tunaendelea na jitihada za kuwaokoa wengine, njia za kupenya hewa na kufika ilipo miili au watu waliobaki zimefunguliwa,” amesema Mhita.
Ajali hiyo ilitokea Agosti 11, 2025 na kuwafukia watu 25 ambao Mpaka sasa walioopolewa ni 10, kati yao watatu wakiwa hai na saba wamefariki dunia.
Post a Comment