HomeHABARI BARAZA LA HABARI TANZANIA LAWAKUTANISHA WAANDISHI WA HABARI NA WANASHERIA MWANZA Misalaba Media August 27, 2025 0 Na Tonny Alphonce - Misalaba MediaWaandishi wa habari mkoa wa Mwanza wamekutanishwa na wanasheria Ili kupitia Sheria zinazowaongoza waandishi wa habari katika shughuli zao za Kila siku.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya Siku Moja , program Meneja wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Josephat Mwanzi amesema ni wajibu waandishi wa habari kujua Sheria zinazowaongoza.Mwanzi amesema MCT imeona ifanye semina hiyo Kwa Wanahabari wa mkoa wa Mwanza Ili wajue namna gani wanaweza kusaidiwa na wanasheria pale wanapopata matatizo ya kisheria."Lengo tunataka kuwasaidia waandishi wajue Sheria zinazowaongoza hasa kipindi hiki Cha uchaguzi Ili waweze kuepuka kuingia kwenye mgogoro na vyombo vya serikali"Amesema MwanziNae program ofisa wa MCT Tumbi Kiganja amewataka waandishi wa chabari wanapata matatizo ya kisheria katika utendaji wao wa kazi kutoa taarifa MCT Ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria."MCT tumekuwa tukirekodi madhila wanayokutananayo waandishi na wengine tumekuwa tukiwapatia msaada huo wakisheria kupitia wanasheria tulionao" amesema KiganjaKARIBU CHUO CHA MADINI SHINYANGA (EARTH SCIENCES INSTITUTE OF SHINYANGA)GUSA LINK HAPA CHINI👇Earth Sciences Institute of Shinyanga (Chuo Cha Madini)APPLICATION PROCESSAPPLICATION FORM🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA You Might Like View all
Post a Comment