" ABIRIA WA MASAFA MAREFU WAPEWA ELIMU YA USALAMA BARABARANI SHINYANGA

ABIRIA WA MASAFA MAREFU WAPEWA ELIMU YA USALAMA BARABARANI SHINYANGA

Abiria wanaosafiri masafa marefu wamepewa elimu ya usalama barabarani ikiwemo kupewa maelekezo ya kufunga mikanda kabla ya kuanza safari pamoja na kuhamasishwa kuwa mabalozi wa usalama barabarani kwa kutoa taarifa pale wanapoona madereva wakivunja sheria za usalama barabarani wakiwa safarini.

Elimu hiyo imetolewa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, katika Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga.

Sajenti Ndimila ameeleza kuwa kila abiria ana jukumu la kuhakikisha usalama wake kwa kuchukua tahadhari za msingi ikiwemo kufunga mikanda na kutokuwa kimya wanapoona dereva anakiuka sheria za usalama barabarani. 

Ameongeza kuwa taarifa za aina hiyo zinasaidia kuokoa maisha na kupunguza ajali ambazo mara nyingi husababishwa na uzembe au uendeshaji holela wa baadhi ya madereva.

Aidha, amewasisitiza abiria wote kuwa walimu kwa kuwaelimisha watu wengine katika maeneo wanakokwenda ili kuendeleza elimu ya usalama barabarani kwa jamii nzima. Ndimila amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza uelewa na kuchochea mshikamano katika kupunguza ajali zisizo za lazima zinazoweza kuepukika endapo kila mmoja atakuwa makini na kuwajibika barabarani.


GUSA LINK HAPA CHINI👇


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 

Post a Comment

Previous Post Next Post