" KATAMBI AREJESHA FOMU ZA UTEUZI KUWANIA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPITIA CCM

KATAMBI AREJESHA FOMU ZA UTEUZI KUWANIA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPITIA CCM

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la shinyanga Mjini Mwl. Ally Mohamed Liuye kushoto akipokea Fomu za uteuzi kutoka kwa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Patrobas Katambi

Na. Elias Gamaya- Shinyanga

Mgombea Ubunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Patrobas Katambi, leo Agosti 27, 2025 anerejesha  Fomu za Uteuzi za kugombea nafasi ya Ubunge zilizotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika ofisi ya Uchaguzi  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

 Mhe. Katambi amerejesha fomu hizo kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Mwl. Ally Mohamed Liuye akiwa ameambatana na viongozi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.

 Ikumbukwe kuwa kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na tume huru ya taifa ya uchaguzi Agosti 28 hadi Oktoba 28 kampeni za uchaguzi zitaanza rasmi kwa Tanzania bara kufitia vyama mbalimbali vya siasa, kwa nafasi ya Rais, Wabunge na Madiwani.



GUSA LINK HAPA CHINI👇


APPLICATION FORM

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 

Post a Comment

Previous Post Next Post