" SMAUJATA YATOA SHUKRANI KWA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM (WMJJWMM) KWA TUZO AMBAZO ZILITOLEWA KWA MWENYEKITI TAIFA SMAUJATA PAMOJA NA TUZO YA CHETI KWA MASHUJAA SMAUJATA TAREHE 26 AGOSTI 2025

SMAUJATA YATOA SHUKRANI KWA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM (WMJJWMM) KWA TUZO AMBAZO ZILITOLEWA KWA MWENYEKITI TAIFA SMAUJATA PAMOJA NA TUZO YA CHETI KWA MASHUJAA SMAUJATA TAREHE 26 AGOSTI 2025

Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) imetoa shukrani kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kutambua mchango wake katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto nchini.

Shukrani hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa SMAUJATA, Shujaa Sospeter Mosewe Bulugu, kufuatia tuzo ya heshima aliyopokea pamoja na cheti cha mashujaa wa SMAUJATA, tarehe 26 Agosti, 2025.

Bulugu amesema wizara hiyo chini ya Waziri Dkt. Dorothy Gwajima na Katibu Mkuu Dkt. John Jingu imekuwa nguzo muhimu katika kuimarisha afua za ustawi wa jamii na ushirikiano na jumuiya hiyo. Amesema wameendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwemo kamati za ulinzi na usalama wa mtoto mtandaoni, uanzishwaji wa madawati ya ulinzi ndani na nje ya shule pamoja na utekelezaji wa mipango ya MTAKUWWA I na MTAKUWWA II.

“Vyeti hivi ambavyo Mashujaa tumevipokea ni chachu ya kuimarisha jitihada zetu na vinaongeza morali ya kusonga mbele zaidi. Uwepo wa SMAUJATA na mchango mkubwa tunaouona unachangiwa na mshikamano wa mashujaa wote wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania,” amesema Bulugu.

Aidha, ametoa pongezi kwa mashujaa wa SMAUJATA nchi nzima akibainisha kuwa kila mmoja kwa nafasi yake amechangia jasho na nguvu hadi jumuiya kufanikisha hatua kubwa iliyofikiwa.

Bulugu pia ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana nao kupitia viongozi na watendaji wake wa ngazi mbalimbali ikiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na Jeshi la Polisi hususan Dawati la Jinsia na Watoto.

Amesema tuzo hiyo kwao ni deni la imani kwa Serikali na taifa kwa ujumla na wamejipanga kuendelea kuchapa kazi kwa kufuata sheria na maelekezo ya taasisi zinazohusika.

GUSA LINK HAPA CHINI👇


APPLICATION FORM

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 

Post a Comment

Previous Post Next Post