" KINJEKITILE MWIRU ATOA WITO WA KAMPENI ZA KISTAARABU KILWA KASKAZINI

KINJEKITILE MWIRU ATOA WITO WA KAMPENI ZA KISTAARABU KILWA KASKAZINI

Na Osama Mohamedi, Misalaba Media - KilwaMgombea ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Kinjekitile Mwilu, ametoa wito kwa wadau wa siasa kuendesha kampeni kwa njia ya kistaarabu, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili ya kisiasa na kuepuka lugha za matusi, kejeli na kashfa.Akizungumza na wananchi mara baada ya kurejesha fomu ya uteuzi katika ofisi za CCM Wilaya ya Kilwa, Kinjekitile alisema anatarajia kuona kampeni safi zinazoakisi ustaarabu wa kisiasa na kuheshimu misingi ya kidemokrasia.“Kampeni ni kipindi cha kushindana hoja na sera, siyo majibizano ya maneno yenye kashfa na kejeli. Naomba vyama vyote tuwe mfano wa siasa safi, ili wananchi wapate nafasi ya kufanya maamuzi kwa misingi ya ukweli na uadilifu,” alisema Kinjekitile.Kinjekitile amewataka wanachama na wapenzi wa CCM kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho kwa Jimbo la Kilwa Kaskazini, unaotarajiwa kufanyika tarehe 06 September katika Kata ya Kipatimu.Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilwa, Ndugu Timami, alitangaza mabadiliko ya ratiba ya uzinduzi wa kampeni, akieleza kuwa mabadiliko hayo ni ya kimkakati na yatazingatia hali halisi ya kisiasa katika jimbo hilo.“Tunapokwenda kuanza rasmi kampeni zetu, tunawaomba wanachama na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi ili kuonesha mshikamano wetu na kuwaunga mkono wagombea wetu,” alisema Timami.Jimbo la Kilwa Kaskazini linatarajiwa kuwa miongoni mwa majimbo yenye ushindani katika uchaguzi huu, huku CCM ikionekana kuweka mikakati ya kuhakikisha inarudisha tena jimbo hilo mikononi mwa chama




GUSA LINK HAPA CHINI👇


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post