MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI, MWL. ALLY LIUYE (kushoto) AKIMKABIDHI FOMU ZA UTEUZI WA MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPITIA CHAMA CHA (TLP). BI. CLARA FRANK MALEKO(kulia)
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mwl. Ally
Liuye leo Oktoba 15, 2025 amekabidhi fomu za uteuzi kwa mgombea wa nafasi ya
Ubunge Bi. Clara Frank Maleko jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia chama cha TANZANIA
LABOUR PARTY (TLP)
Bi. Clara anakuwa mgombea wa pili kuchukua fomu za
Uteuzi kugombea ubunge kwa jimbo la Shinyanga Mjini ambapo jumla ya vyama
11 vilivyosajiliwa kwa jimbo hili vinatarajiwa kushiriki katika mchakato huo.
Zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi ya Ubunge umeanza
rasmi hapo jana Agosti 14, 2025 ambapo linatarajiwa kutamatika Agosti 27, 2025
ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, utakaofanyika Oktoba 29,
2025.
Post a Comment