MSIMAMIZI MSAIDIZI WA UCHAGUZI WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI,
NDG. PERES KAMUGISHA (kushoto) AKIMKABIDHI FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO
LA SHINYANGA MJINI BI. MERYESTER NYARUSANDA ALPHONCE KUPITIA CHAMA CHA (CCK) (kulia)
NA. ELIAS GAMAYA- SHINYANGA
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Ndg. Peres Kamugisha leo Oktoba 15, 2025 amekabidhi fomu za uteuzi mgombea wa nafasi ya Ubunge Bi. Meryester Nyarusanda Alphonce jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia CHAMA CHA KIJAMII (CCK)
Bi. Meryester anakuwa mgombea wa tatu kuchukua fomu za Uteuzi kugombea ubunge kwa jimbo la Shinyanga Mjini ambapo jumla ya vyama 11 vilivyosajiliwa kwa jimbo hili vinatarajiwa kushiriki katika mchakato huo.
Zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi ya Ubunge umeanza rasmi hapo jana Agosti 14, 2025 ambapo linatarajiwa kutamatika Agosti 27, 2025 ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Post a Comment