" CCM YAWAPITISHA WAGOMBEA UBUNGE MKOA WA SHINYANGA

CCM YAWAPITISHA WAGOMBEA UBUNGE MKOA WA SHINYANGA




Na Mapuli Kitina Misalaba

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Agosti 23, 2025 imewapitisha rasmi wagombea wa ubunge watakaoiwakilisha katika majimbo ya mkoa wa Shinyanga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Kikao hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, kimehitimisha mchakato ulioanza Juni 28, 2025 kupitia hatua za uchukuaji na urejeshaji fomu, kura za maoni na sasa uteuzi wa mwisho.

Kwa mujibu wa majina yaliyopitishwa, wagombea wa CCM mkoa wa Shinyanga ni:

  1. Patrobas Katambi – Jimbo la Shinyanga Mjini

  2. Benjamin Lukubha Ngayiwa – Jimbo la Kahama Mjini

  3. Mabula J. Magangila – Jimbo la Msalala

  4. Ahmed Salum – Jimbo la Solwa

  5. Azza Hillal Hamad – Jimbo la Itwangi

  6. Emmanuel Cherehani – Jimbo la Ushetu

  7. Lucy Mayenga – Jimbo la Kishapu

Watakaopitishwa sasa wanakabidhiwa jukumu la kupeperusha bendera ya CCM katika kampeni za uchaguzi mkuu zitakazoanza Agosti 28 na kumalizika Oktoba 28, 2025.

Kwa upande wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), dirisha la kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hizo litafungwa Agosti 27, siku moja kabla ya kuanza rasmi kampeni.

Aidha, kikao hicho cha Halmashauri Kuu kinatarajiwa pia kumpa chama Katibu Mkuu mpya kufuatia Dk Emmanuel Nchimbi kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa CCM, nafasi inayompa Mwenyekiti wa chama nafasi ya kupendekeza jina jingine kwa ajili ya uteuzi huo.


GUSA LINK HAPA CHINI👇


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post