" JOHN KATELE APONGEZWA UDIWANI KATA YA PANGANI

JOHN KATELE APONGEZWA UDIWANI KATA YA PANGANI

PANGANI, Kibaha Mjini


Shangwe na matumaini mapya yameibuka katika Kata ya Pangani baada ya John Katele kuchukua hatua ya kwanza muhimu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuteuliwa kuingia katika mchujo wa kura za maoni kuelekea kugombea Udiwani.

Wananchi na wanachama wa CCM wameonyesha imani kubwa kwa Katele, wakisema hatua hii inaashiria mwanzo wa mabadiliko chanya katika kata hiyo.

"Uteuzi huu wa awali ni dalili kwamba vijana na viongozi wenye maono wanapewa nafasi. Tunaamini Katele ataendelea kushirikiana nasi kuhakikisha changamoto zetu zinapata suluhu," alisema Bw. Ramadhan Saidi, mkazi wa Ubafu.

Wanawake na vijana wa kata hiyo wamesema wako tayari kujitokeza kwa wingi kumpa kura katika kura za maoni, wakimtaja Katele kuwa kiongozi mwenye dira na mshikamano wa kijamii.


"Ni kiongozi wa wananchi na mwenye nguvu ya kushirikisha watu wote bila kujali tofauti zao. Tunamwamini," alisema Bi. Asha Mbwana wa Mtaa wa Lumumba.

Katele anasifika kwa utulivu na hekima pamoja na mtandao mzuri wa kuweza kuwafikia wakubwa mbalimbali, kama mojawapo ya mbinu ya kuzipatia majibu changamoto za wananchi wa Pangani.

"Pangani ina changamoto nyingi, tunataka Diwani ambaye ana uhusiano mzuri na watu, diwani ambaye ana hali ya utulivu wa akili," anasema Hamida Juma, mkazi wa Ubafu. Kura za maoni za CCM zimepangwa kufanyika hivi tarehe 4 Agosti, na uteuzi wa awali wa Katele unatazamwa kama hatua ya kihistoria kwa safari yake ya kisiasa ndani ya chama hicho tawala.

Post a Comment

Previous Post Next Post