Na Lydia Lugakila
Kagera
Evance Kamenge ambaye ni mdau wa maendeleo mchumi na mkulima kutoka mkoani Kagera ambaye pia amekuwa akijihusisha na masuala mbali mbali ya kisiasa amewataka watia nia katika nafasi za ubunge mkoani Kagera ambao hawakufanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha ubunge kutochukia ushindani, bali watumie hali hiyo kuwajenge na kuwaondoa katika manunguniko ya aina yoyote ili kulinda amani ya nchi yao.
Kamenge ametoa kauli hiyo kupitia vyombo vya ambapo amesema kuwa wote walioshinda kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wamepita kwenye mchujo, na wanapaswa kukumbuka kwamba utawala wowote unatoka kwa Mungu hivyo, wale waliokosa nafasi hiyo wasiwe chanzo cha kuleta mkwamo ndani ya chama wala katika jamii.
Mchumi huyo amewashauri waliopata nafasi na kuaminiwa na wajumbe pamoja na chama, kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia wananchi kwa kurudisha kile ambacho wananchi wanahitaji.
"Nawaomba wananchi na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuitunza amani, kwani ndilo jambo pekee ambalo Waafrika wanajivunia," alisema Kamenge.
Kwa kuzingatia umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi na wananchi Kamenge amesisitiza kwamba ni lazima jamii ibebe jukumu la kujenga nguvu na mshikamano ili kufanikisha maendeleo.
Kamenge si tu mchumi, bali pia ni mdau wa maendeleo ambaye hivi karibuni amechukua hatua za kutia nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Missenyi, Kagera, ingawa hakubahatika kufanikiwa.
Hivi karibuni Kamenge amekuwa akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi na wananchi, akiwashauri waliopata nafasi za uongozi kutimiza wajibu wao kwa jamii.
Aidha ametoa wito kwa kila mmoja kuwa na jukumu katika kujenga jamii imara na yenye mshikamano, akisisitiza juu ya umuhimu wa kuanzisha miradi ya kijamii ambayo itasaidia jamii na kuongeza ajira, pamoja na kuimarisha uchumi wa maeneo mbalimbali nchini.
Hata hivyo ameongeza kuwa amani ni jambo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi hivyo inapaswa kulindwa kwa gharama yoyote.
GUSA LINK HAPA CHINI👇
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment