HAYA NI MATOKEO AMBAYO SIYO RASMI
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, ameibuka mshindi wa kishindo katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Shinyanga Mjini baada ya kujizolea kura 2,922, akimshinda kwa mbali aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo Stephen Masele aliyepata kura 874 pekee.
Takwimu kutoka kila kata zinaonesha ushindi mpana kwa Katambi, akiongoza katika maeneo yote 17 yaliyopiga kura:
MATOKEO YA KATA KWA KATA:
- Ibadakuli – Katambi: 337 | Masele: 47
- Old Shinyanga – Katambi: 220 | Masele: 8
- Kizumbi – Katambi: 275 | Masele: 28
- Kolandoto – Katambi: 253 | Masele: 146
- Mwawaza – Katambi: 210 | Masele: 52
- Chibe – Katambi: 179 | Masele: 24
- Mwamalili – Katambi: 178 | Masele: 16
- Lubaga – Katambi: 174 | Masele: 30
- Ndembezi – Katambi: 161 | Masele: 117
- Kitangili – Katambi: 156 | Masele: 96
- Kambarage – Katambi: 144 | Masele: 60
- Ibinzamata – Katambi: 133 | Masele: 8
- Ngokolo – Katambi: 128 | Masele: 78
- Chamaguha – Katambi: 123 | Masele: 23
- Masekelo – Katambi: 113 | Masele: 48
- Ndala – Katambi: 96 | Masele: 35
- Mjini – Katambi: 59 | Masele: 57
UDIWANI: WANAOPEWA HONGERA
Katika nafasi za udiwani kwa baadhi ya kata, wanachama hawa wa CCM wameibuka kidedea na kupongezwa na wanachama wa maeneo yao:
✅ Jackline Isalo – Ngokolo
✅ Pendo Sawa – Ndembezi
✅ Hamis Hadji – Kambarage
✅ Jonathan Madete – Kitangili
✅ Mh. Zamda – Ndala
✅ Salum Kitumbo – Mjini
✅ Edwin Washa – Mwawaza
MISALABA MEDIA itaendelea kukuletea taarifa za kina kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
Post a Comment